Jina la (IUPAC) | |
---|---|
4-{8-Amino-3-[(2S)-1-(2-butynoyl)-2-pyrrolidinyl]imidazo[1,5-a]pyrazin-1-yl}-N-(2-pyridinyl)benzamide | |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Calquence |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
MedlinePlus | a618004 |
Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
Kategoria ya ujauzito | C(AU) ?(US) |
Hali ya kisheria | Prescription Only (S4) (AU) ℞-only (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Kwa mdomo |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Visawe | ACP-196 |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C26H23N7O2 |
|
Acalabrutinib, inayouzwa kwa jina la chapa Calquence, ni dawa inayotumika kutibu lymphoma ya seli ya mshipa (MCL) na leukemia sugu ya lymphocytic (CLL).[1][2] Kwa CLL inaweza kutumika mwanzoni au kwa wale ambao wameshindwa matibabu mengine.[2] Inachukuliwa kwa mdomo.[3]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuumwa na kichwa, kuhisi uchovu, chembechembe nyekundu za damu kupungua, chembechembe nyeupe za damu kidogo na chembechembe za kugandisha damu kidogo.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha maambukizi, kutokwa na damu, saratani zaidi, na mpapatiko wa atiria.[3] Matumizi yake wakati wa ujauzito yanaweza kumdhuru mtoto.[3] Ni kizuizi cha tyrosine kinase cha Bruton, ambacho hupunguza kasi ya mkusanyiko wa seli za B za saratani.[2]
Acalabrutinib iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2017 na Ulaya mwaka wa 2020.[1][2] Nchini Uingereza, mwezi mmoja wa dawa hii uligharimu NHS takriban £5,100 kufikia mwaka wa 2021.[4] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 15,000 za Marekani.[5]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Text was copied from this source which is © European Medicines Agency. Reproduction is authorized provided the source is acknowledged.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)