Adam Monroe

Adam Monroe/Takezo Kensei
muhusika wa Heroes

David Anders kama Adam Monroe
Mwonekano wa kwanza "Four Months Later..."
Mwonekano wa mwisho "Dying of the Light" (Adam wa kweli)
"Pass/Fail" (katika mauzauza ya Hiro)
Imechezwa na David Anders
Maelezo
Majina mengine Takezo Kensei
UwezoKujitengeneza seli upya kwa haraka zaidi

Adam Monroe, pia anajulikana kama Takezo Kensei (剣聖 武蔵 - Kensei Takezō) katika Japani yenye mgogoro, ni jina la kutaja uhusika uliochezwa na David Anders kwenye mfululizo wa kipindi cha televisheni cha Heroes kinachorushwa hewani na kituo cha TV cha NBC. Muhusika huyu alianza kuonekana kwa mara ya kwanza katika sehemu ya "Four Months Later..." ya msimu wa pili wa mfululizo, japokuwa hekaya za Kensei zimekuwa zikitajwa mara kwa mara katika msimu wa kwanza. Kipawa chake cha kujitengeneza upya kumesimamisha kukua kwa umri wake, unamfanya aonekane katika karne za kale na za sasa katika mfululizo. Yeye ni adui mkubwa wakati wa msimu wa pili.

Muhtasari wa muhusika

[hariri | hariri chanzo]

Takezo Kensei

[hariri | hariri chanzo]

Jina la "Kensei" linamaanisha "Mtakatifu wa Upanga" na "Takezo" ni jina la kihistoria la bwanapanga Miyamoto Musashi – Kensei linatokana na hekaya kadha wa kadha za watalaamu wa kupambana kwa mapanga wa Kijapani, hiyo ikiwa pamoja na Musashi.[1] Kulingana na hekaya, Kensei alikuwa mshujaa wa Kijapani, anafahamika zaidi kwa kuiokoa Japani kutoka kwa "White Beard" (白髭 Shirohige?) katika karne ya 17. Hata hivyo, anajithibitisha kuwa ni Mwingereza aliyekuja Japani kujitafutia riziki.

Hiro anataja hekaya za Takezo Kensei mara kibao katika msimu wa kwanza, ilihusiana kiasi tu hadi hapo alipokuja kufundishwa kendo na baba yake katika sehemu ya "Landslide". Awali, katika "Godsend" na "The Fix", Hiro amesema kwamba ule upanga – ambao alikuwa akihangaikia kuuiba kutoka kwa Mr. Linderman – umemsaidia Kensei kuzingatia nguvu zake. Pia amesema kwamba baba yake amekuwa akimwambia hadithi za Kensei, huenda ni pamoja na Hiro kumwambia Kensei mara kwa mara katika msimu wa pili. Wakati anafunzwa na baba yake kwa ajili ya sehemu yake ya "Saving the World" kabla ya mtiti na Sylar huko mjini New York, Hiro anahusisha hadithi ya "Kensei and the Dragon" na kutambua kwamba, ikiwa anataka kushinda, hana budi kuwa na nguvu za kutosha ikiwa hata kujitoa muhanga.

  1. "Behind the Eclipse: "Heroes" Week Sixteen"". CBR. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-11. Iliwekwa mnamo 2007-10-13.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]