Adelaida Kleti Semesi, pia Adelaide K. Semesi (1951 – 6 Februari 2001),[1] alikuwa mtaalamu wa ikolojia kutoka nchini Tanzania. Adelaida alipata kuwa Profesa wa Viumbe Bahari katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Ambapo alijikita zaidi katika ekolojia ya mikoko. Sifa kubwa ya Semesi ni kuwa mwanamke wa kwanza kuwa profesa katika uwanja wa sayansi asilia nchini Tanzania.
Semesi alizaliwa mwaka 1951 huko Haubi, Tanzania.[2] Alimaliza shahada ya kwanza ya Sayansi (BSc) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1975,[2] na kisha kupata shahada ya uzamivu (PhD) kutoka taasisi hiyo hiyo mwaka 1979.[3]
Semesi alianza kufundisha mwaka 1975 akiwa kama msaidizi. Akafikia hadhi ya uprofesa hadi alipofariki.[2] Mwaka wa1982, alianzisha mpango wa utafiti kuhusu ufugaji mwani huko Zanzibar; matokeo yake yalisababisha uwekezaji mkubwa zaidi katika sekta hiyo, ambayo ilitoa ajira pana zaidi, hasa kwa wanawake.[2] Kazi yake kuhusu ekolojia ya mikoko ilianza mwaka 1990, na Tanzania ikawa moja ya nchi za mwanzo kuwa na mpango wa usimamizi wa mazingira kwa mikoko.[1] Pia alikuwa mtetezi wa maarifa ya kiasili yanayowasilishwa kwa njia ya mdomo. Alisisitiza zaidi matumizi yake ndani ya jamii, hasa yanayohusiana na nyanja za kilimo.[4]
Alipachikwa jina la "mama mikoko",[5][6] alibobea katika ekolojia ya mikoko,[5] alikuwa Mjumbe wa Baraza la Kimataifa la Ekolojia ya Mikoko,[1] Mjumbe wa Baraza la Jumuia ya Mikoko,[7] na mwanachama wa bodi ya wadhamini ya Western Indian Ocean Marine Science Association.[6]
Semesi alikuwa profesa wa kwanza mwanamke nchini Tanzania katika nyanja ya sayansi asilia.[6] Licha ya ubaguzi dhidi ya wanawake katika sayansi, alitambuliwa kwa wingi wa tuzo za kimataifa.[8] Tuzo hizo zilijumuisha ufadhili wa Fulbright katika Chuo Kikuu cha South Florida mwaka 1982, ambapo alifanya utafiti uitwao "Analysis of Certain Marine Phycocolloids".[9] Alipokea tuzo ya Pew Trust mwaka 1992, ambayo aliitumia kufanya utafiti mkubwa kuhusu eneo la Bagamoyo, ikijumuisha vyanzo vya baharini, takwimu za kijamii na kiuchumi na mambo mengine.[7]
Wakati wa kifo chake, Semesi alikuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Sayansi ya Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.[10] Alifariki tarehe 6 Februari 2001.[1] Kifo chake kilielezewa katika Pwani Yetu: The Newsletter of the Tanzania Coastal Management Partnership kama "hasara kubwa kwa uhifadhi wa mazingira ya bahari".[10]
Collen, J., M. Mtolera, K. Abrahamsson, A. Semesi and M. Pedersen. 1995. Farming and physiology of the red algae Eucheuma: Growing commercial importance in East Africa. Ambio 24(7): 497-450
Mtolera, M.S.P., J. Collen and A.K. Semesi. 1995. Destructive hydrogen peroxide production in Eucheuma denticulatum (Rhodophyta) during stress caused by elevated pH, high light intensities and competition with other species. olera, M.S.P., J. Collen and A.K. Semesi. 1995. Destructive hydrogen peroxide production in Eucheuma denticulatum 30(4): 289
Semesi A.K. 1993. Wetlands of sub-saharan Africa, their relevance and management. Proceedings of the conference on water and environment: Key to Africa's Development 151-164
Engdahl, S., F. Mamboya, M. Mtolera, A. Semesi and M. Björk. 1998. The brown macroalgae Pakina boergesenii as an indicator of heavy metal contamination in the Zanzibar Channel. Ambio 27(8): 694-700
Semesi, A.K. 1998. Coastal resources utilization and conservation issues in Bagamoyo, Tanzania. Ambio 27(8): 635-644
Semesi, A.K. 1998. Mangrove management and utilization in Eastern Africa. Ambio 27(8): 620-626
Mtolera, M.S.P., J. Collen and A.K. Semesi. 1996. Stressed-induced production of volatile halogenated organic compounds in Eucheuma denticulatum (Rhodophyta) caused by elevated pH and high light intensities. European Journal of Phycology 31(1): 91
Bjork, M., S.M. Mohammed and A. Semesi. 1995. Coralline algae, important coral-reef builders threatened by pollution. Ambio 24(7): 502
↑Nyika, E.A.; Ngusaru, A.S.; Mmochi, A. J. (2000). Directory of Marine Scientists Working in Tanzania(PDF). Tanzania Coastal Management Partnership. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo(PDF) mnamo 2024-03-18. Iliwekwa mnamo 2024-09-07.