Anselmo Zarza Bernal (4 Juni 1916 – 15 Aprili 2014) alikuwa askofu wa Meksiko katika Kanisa Katoliki.
Bernal alizaliwa mjini Atlixco, Puebla mnamo Juni 1916 akapadrishwa mwaka 1939. Alihudumu kama Askofu wa Linares, Nuevo León, kuanzia 1962 hadi 1966, na baadaye kama Askofu wa León, Guanajuato, kuanzia 1966 hadi 1992.
Bernal alifariki mjini León, Guanajuato mnamo Aprili 2014 akiwa na umri wa miaka 97.
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |