Atiak

Ramani ya Uganda, Atiak hupatikana katika majiranukta
3 ° 15'33.0 "Kas, 32 ° 07'23.0" Mash.

Atiak ni mji katika Mkoa wa Kaskazini wa Uganda, kando ya Barabara ya Gulu-Nimule ambayo ilikuwa njia kuu ya biashara kati ya Uganda na Sudan Kusini.

Mahali ilipo

[hariri | hariri chanzo]

Atiak iko katika kaunti ya Kilak ndani ya Wilaya ya Amuru, takriban kilomita 71 kwa mwendo wa barabara, kaskazini mwa Gulu ambao ndiyo mji mkubwa zaidi katika mkoa mdogo wa Acholi.[1] Atiak ipo umbali wa takribani kilomita 35 kusini mwa mji wa Sudan Kusini wa Nimule katika mpaka na Uganda.[2] Hii ni takriban kilomita 407 kutoka kaskazini mwa Kampala, jiji kubwa zaidi.[3] Majira nukta ni (3 ° 15'33.0 "Kas, 32 ° 07'23.0" Mash. (Latitudo: 3.259167; Longitudo: 32.123056))


  1. GFC (23 Julai 2015). "Road Distance Between Atiak And Gulu With Map". Globefeed.com (GFC). Iliwekwa mnamo 23 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. UNRA. "Atiak-Nimule Road (35Km): Funded By JICA And Government of Uganda". Uganda National Roads Authority (UNRA).
  3. GFC (23 Julai 2015). "Road Distance Between Kampala And Gulu With Map". Globefeed.com (GFC). Iliwekwa mnamo 23 Julai 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)