Austregesili (pia: Austregisilus, Outrille, Aoustrille; 551 hivi - 11 Septemba 624 hivi) anakumbukwa kama askofu wa Bourges (Ufaransa) kuanzia mwaka 612 hadi kifo chake.
Baada ya kufanya kazi katika ikulu, alikwenda kujiunga na monasteri akawa abati hadi alipoteuliwa kuwa askofu.
Hapo alionyesha upendo wa pekee kwa maskini, mayatima, wagonjwa na waliohukumiwa kufa[1].
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 20 Mei[2][3][4].
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |