Jamarr Antonio Stamps (alijulikana zaidi kwa jina la kisanii kama Bad Azz; 27 Novemba 1975 – 11 Novemba 2019) alikuwa rapa wa Marekani na mwanachama wa kundi la Tha Dogg Pound Gangsta Crips, ambalo linajulikana pia kama DPGC.
Alizaliwa Hawaiian Gardens, California, California, Marekani akaanza kazi yake ya kurap kwenye tamasha za nyumbani na kujunga na kundi la LBC Crew. Baada ya kuwa na ubeti wa msanii mgeni kwenye wimbo wa Tupac "Krazy" mnamo 1996 alikuwa amejitayarisha kusainiwa kwa lebo ya kurekodi muziki iliyopendekezwa na Tupac, Makaveli Records. Baada ya kusainiwa kwa kifupi katika lebo ya Snoop Dogg ya Doggystyle Records, Bad Azz alifanya maonyesho kadhaa ya kigeni kabla ya kulimbukia lebo ya Priority Records mnamo 1998 na albamu ya Word on tha Streets.
Mnamo mwaka wa 2001, alifuatilia na albamu ya Personal Business ambayo single ya "Wrong Idea" (iliyowasirikisha Snoop Dogg, Kokane, na Lil '½ Dead) ilifikia #75 kwenye chati ya Hot R&B/Hip-Hop Songs.
Mnamo mwaka wa 2009, aliachia albamu akiwa Bizzy Bone, "Thug Pound." Katika msimu wa majira ya joto wa 2010, aliangusha single mpya ya For As Long As I Can. Mnamo Machi 2013 Bad Azz alipigana na binamu wa Snoop Dogg, Ray J, Bad Azz alisema ilikua ni kulipiza kisasi kwa kupigwa na Suge Knight na msafara wake muongo mmoja uliopita.
Mnamo mwaka wa 2011, alitokea kwenye albamu ambayo haikuzingatiwa kama albamu ya Haven't You Heard?(We Givin' Something Bacc To Tha Street) ambayo ilitolewa na lebo za Death Row Records na WideAwake mnamo Februari 8, 2011.
Mnamo mwaka 2014, Bad Azz aliachia video ya muziki ya wimbo uliopewa jina la "Baby Wut'z Up", akishirikiana na Turf Talk, alitangaza jina la albamu mpya The Nu Adventures of Bad Azz, ambayo ilitolewa mnamo 2018.
Mnamo Novemba 11, 2019, msanii Daz Dillinger alithibitisha kwenye media za kijamii kuwa Bad Azz alikuwa amefariki akiwa na umri wa miaka 43.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bad Azz (rapper) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |