Ben Pol | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Bernard Michael Paul Mnyang’anga |
Pia anajulikana kama | Ben Pol |
Amezaliwa | 8 Septemba 1989 Dar es salaam |
Kazi yake | Mwimbaji Mwigizaji |
Ala | Sauti |
Miaka ya kazi | 2009-hadi sasa |
Ameshirikiana na | Darassa, Saida Karoli, Belle 9 |
Bernard Michael Paul Mnyang’anga (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Ben Pol; amezaliwa 8 Septemba 1989) ni msanii wa muziki wa kizazi kipya na mwigizaji kutoka nchini Tanzania. Hasa anaimba muziki wa R&B.
Ben Pol alianza kujulikana mnamo mwaka 2010 baada ya kutoa kibao cha "Nikikupata" ambacho kiliweza kumtambulisha katika ulimwengu wa Bongo Flava. Kwa asili Ben ni mtu wa Dodoma[1], tena anajisifu kama mtu kutoka kanda ya kati.
Baadaye akaja kutamba zaidi na vibao kama vile
Upande wa filamu, amepata kucheza katika filamu ya Sunshine na baadhi tu ya filamu zilizokuwa chini ya MFDI Tanzania na kuongozwa na Karabani.[2]
Ameshinda tuzo za mziki Tanzania (KTMA) Kwa miaka mitatu mfululizo kudhibitisha ubora wake katika muziki wa R&B.
Ameshinda tuzo za www.mdundo.com
Tuzo za hipipo Uganda
Makala hii kuhusu mwanamuziki/wanamuziki fulani wa Tanzania bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Ben Pol kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |