Bernadi wa Parma (Firenze, Italia, 1060 hivi – Parma, Italia, 4 Desemba 1133) alikuwa mmonaki na mkuu wa urekebisho wa Wabenedikto wakaapweke wa Vallombrosa.
Alifanywa kardinali na askofu wa Parma kuanzia mwaka 1106 hadi kifo chake.
Daima alijitahidi kama mmonaki kulenga ukamilifu wa Kikristo, kama kardinali kulenga ustawi wa Kanisa na kama askofu kulenga wokovu wa watu [1].
Tangu wakati huo aliheshimiwa kama mtakatifu. Mwaka 1139 Papa Inosenti II alithibitisha sifa hiyo [2].
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 4 Desemba[3].
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link){{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link){{cite book}}
: CS1 maint: unrecognized language (link)