Bernardo Calvo

Mt. Bernardo Calvo alivyochorwa.

Bernardo Calvo, O.Cist. (kwa Kikatalunya: Bernat Calvó; Mas Calvó, 1180 hivi - Vic, 26 Oktoba 1243) alikuwa hakimu kaskazini mashariki mwa Hispania ya leo, lakini mwaka 1214 aliacha kazi hiyo akajiunga na monasteri ya Wasitoo ya Misalaba Mitakatifu akawa abati wake.

Kisha kuchaguliwa kuwa askofu wa Vic (1233) alijitahidi sana kutetea imani sahihi na kueneza Ukristo nchini [1]

Alitangazwa mwenye heri na Papa Aleksanda IV mwaka 1260 halafu mtakatifu na Papa Klementi XI tarehe 26 Septemba 1710.

Sikukuu yake huadhimishwa kila tarehe 25 Oktoba[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • Burns, Robert Ignatius. The Crusader Kingdom of Valencia: Reconstruction on a Thirteenth-Century Frontier. Cambridge, Massachusetts: Harvard University Press, 1967. See page 309.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.