Brian Maxine

Brian Maxine (alijulikana kwa jina la Goldbelt, 13 Agosti 193813 Novemba 2024) alikuwa mchezaji wa mieleka na msanii wa kabare kutoka Uingereza. Alishikilia taji la Uingereza la Welterweight kuanzia mwaka 1969 hadi 1971. Katika mwaka 1971, alishinda taji la Uingereza la Middleweight, na kwa kushikilia mataji haya mawili kwa pamoja kwa muda mfupi, alikua bingwa wa kwanza mwenye mataji mawili ya uzito tofauti kwa wakati mmoja, ambayo ni jambo la kipekee katika historia ya mieleka nchini Uingereza baada ya vita vya pili vya dunia. [1]

  1. "Wrestling Titles.com website with full history of British Welterweight Championship". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 30 Oktoba 2016. Iliwekwa mnamo 7 Novemba 2010.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Brian Maxine kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.