Butiama | |
Mahali pa mji wa Butiama katika Tanzania |
|
Majiranukta: 1°46′12″S 33°58′12″E / 1.77000°S 33.97000°E | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Mara |
Wilaya | Butiama |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 24,871 |
Butiama ni mji mdogo ulio makao makuu ya wilaya ya Butiama katika Mkoa wa Mara (Tanzania) yenye postikodi namba 31201. Uko karibu na Ziwa Viktoria.
Wakazi asilia ni kabila la Wazanaki.
Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 24,871 [1]. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 19,217 waishio humo.[2]
Wilaya ya Butiama ilianzishwa rasmi mnamo Machi 2012.
Butiama imejulikana kimataifa kwa sababu ni mahali ambako alizaliwa rais wa kwanza wa Tanganyika halafu wa Tanzania, Julius Nyerere. Aliendelea kuwa na nyumba kijijini alikorudi baada ya kustaafu kama rais na baadaye pia kama mwenyekiti wa chama tawala cha CCM. Baada ya kufariki kwake (London 14 Oktoba 1999), makazi yake yamekuwa jumba la Makumbusho. Pia kaburi lake liko katika kijiji cha Butiama.
Kuna pia meli inayoitwa "Butiama" inayozunguka ziwani kati ya Mwanza na Ukerewe.
Kata za Wilaya ya Butiama - Mkoa wa Mara - Tanzania |
||
---|---|---|
Bisumwa | Buhemba | Bukabwa | Buruma | Busegwe | Buswahili | Butiama | Butuguri | Bwiregi | Kamumegi | Kukirango | Kyanyari | Masaba | Mirwa | Muriaza | Nyamimange | Nyankanga | Sirorisimba |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Butiama kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |