"C U When U Get There" ni wimbo wa Coolio akiwa na 40 Thevz. Wimbo mzima umechukua sampuli ya Johann Pachelbel katika tungo yake ya Canon katika D Major. Wimbo ulitolewa mnamo mwaka 1997 ukiwa kama single ya kwanza kutoka katika albamu ya Coolio My Soul. "C U When U Get There" vilevile ulionekana kama kibwagizo cha filamu ya mwaka wa 1997, Nothing to Lose. Wimbo ulishika nafasi ya 12 kwenye chati za Billboard Hot 100 na nafasi ya 7 kwenye chati za Hot Rap Tracks nchini Marekani. Vilevile ulipata mafanikio kimataifa, kwa kushika nafasi ya 10 katika kibao za Ulaya. Wimbo umechukua sampuli ya Pachelbel's Canon kwa kila kitu. Rekodi hii ilizadiwa dhahabu na RIAA.
↑"Billboard Top 100 - 1997". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-06-11. Iliwekwa mnamo 2010-08-28. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)