Camarata ilikuwa bandari ya Karthago na ya Dola la Roma kando ya Bahari ya Kati karibu na Siga nchini Mauretania. Chini ya Warumi, ilikuwa sehemu ya mkoa wa Mauretania Caesariensis. Mabaki yake yanadhaniwa kuwa yale kwenye mdomo wa Wadi Ghazer[1] Jijini Djeloul Sidi Safi, Algeria.[2] Mji wa baharini ulikuwa karibu na Siga.[3]
Camarata ilitoa sarafu za shaba zilizopigwa chapa na jina la mji kwa lugha ya Kipunik na picha duni ya kichwa upande wa mbele na zabibu na masuke ya ngano upande wa nyuma. Imehusishwa na Zimran] au kuelezwa kama nchi ya Zimrite pamoja na Thamarita na Tumarra.[4]
Baada ya uvamizi wa Kifaransa wa Algeria, eneo karibu na Camarata ilijulikana kwa madini yake bora ya chuma.[5]
{{citation}}
: CS1 maint: location missing publisher (link).
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Camarata (Mauretania) kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |