Cetrorelix

Cetrorelix, inayouzwa kwa jina la chapa Cetrotide, ni dawa inayotumika katika matibabu ya uwezo wa kushika mimba ili kuzuia kudondoshwa kwa yai mapema kwa wanawake wanaopata kichocheo cha ovari.[1] Dawa hii inatolewa kwa njia ya kudungwa sindano chini ya ngozi.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na ugonjwa wa kupata hisia za kupita kiasi homoni za ovari zinpozidi (ovari hyperstimulation syndrome), kichefuchefu, na maumivu ya kichwa.[3] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha hisia za mzio mkali unaoweza kutishia maisha (anaphylaxis) na matatizo ya ini.[3] Matumizi yake wakati wa ujauzito inaweza kumdhuru mtoto.[3] Ni kizuizi kinachozuia utoaji wa homoni ya gonadotropini (GnRH).[3]

Cetrorelix iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu huko Ulaya mwaka wa 1999 na Marekani mwaka wa 2000.[1][3] Nchini Uingereza, maikrogramu 250 hugharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £27 kufikia mwaka wa 2021.[2] Kiasi hiki nchini Marekani kinagharimu takriban dola 250 za Kimarekani.[4]

  1. 1.0 1.1 "Cetrotide". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 16 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 778. ISBN 978-0857114105.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 "Cetrorelix Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Februari 2021. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Cetrorelix Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 3 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Cetrorelix kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.