Charity Kaluki Ngilu (alizaliwa mnamo mwaka 1952) ni gavana wa Kaunti ya Kitui. Alikuwa waziri wa afya katika serikali ya rais Mwai Kibaki kuanzia mwaka 2002 hadi 2007.
Ngilu alizaliwa katika wilaya ya Makueni, Ukamba, mwaka 1952. Alifanya kazi na Benki Kuu ya Kenya hadi kuanzisha kampuni yake ya vifaa vya plastiki. Aliolewa na Michael Mwendwa Ngilu aliyeaga dunia mwaka 2006. Amezaa watoto watatu.
Aliingia katika siasa ya upinzani mwaka 1991, aligombea na kushindi kiti cha mbunge wa Kitui Kati kwa chama cha Democratic Party (DP) cha Mwai Kibaki.
Mwaka 1997 aliondoka katika DP akiandaa kugombea urais yeye mwenyewe akiwa mwanamke wa kwanza nchini wa kugombea urais. Akajiunga na chama cha SDP akamaliza nafasi ya tano.[1]
Baadaye akajiunga na National Party of Kenya akashiriki katika maungano ya upinzani ya NAK kwa uchaguzi wa 2002. NAK iliunga mkono na LDP ya Raila Odinga kuwa NARC.
Ngilu alikuwa mwenyekiti wa chama kipya cha National Alliance of Rainbow (NARC) akajipatia jina la "Mama Rainbow".
Katika serikali ya KIbaki alikuwa waziri wa afya.
Oktoba 2007 alitangaza kusimama upande wa ODM akaachishwa katika serikali.
Alirudishwa bungeni mwaka 2007 kwa tiketi ya NARC.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Charity Ngilu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |