Chase Edmunds | |
---|---|
muhusika wa 24 | |
James Badge Dale kama Chase Edmunds | |
Imechezwa na | James Badge Dale |
Msimu | 3 |
Maelezo |
Chase Edmunds ni jina la kutaja uhusika wa kipindi cha televisheni cha Kimarekani cha 24. Uhusika ulichezwa na James Badge Dale. Huyu alikuwa na cheo kikubwa sana katika Kitengo cha Kuzuia Ugaidi cha Los Angeles (CTU).[1]
Alianza kuonekana katika 24: The Game akiwa kama muhusika wa gemu tu, lakini baadaye akajakuonekana tena katika msimu wa tatu au Siku ya 3, akiwa kama msaidizi wa Bauer, na anamahusiano ya kimapenzi na binti wa Bauer, Kim Bauer. Chase ni mchapa kazi. Chase ni muhusika pekee aliyeweza kumudu nafasi ya Jack kuliko muhusika mwingine yeyote yule aliyeonekana katika mfululizo huu wa 24.