Chuo Kikuu cha Muhimbili | |
---|---|
Kimeanzishwa | 1963 |
Aina | Chuo kikuu cha umma |
Mwenyekiti | Mariam Mwafisi |
Chansela | Ali Hassan Mwinyi |
Walimu | 306 |
Wanafunzi | 3,861 |
Mahali | Dar es Salaam, Tanzania |
Tovuti | muhas.ac.tz |
Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (kwa Kiingereza: Muhimbili University of Health and Allied Sciences; kifupi: MUHAS) chuo kikuu cha umma kilichopo Dar es Salaam, Tanzania. Ni taasisi kubwa ya afya na elimu ya afya huko Dar es Salaam Tanzania.
Kilipewa hadhi ya kuwa chuo kikuu mwaka 2007[1] Kabla ya hapo, kama Chuo cha Elimu ya Afya kilikuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Neno Muhimbili limetokana na neno la Kizaramo "mibili" likimaanisha kiungo cha mtoto tumboni na mama yake (plasenta) Hospitali ilipoanza Wazaramo walisema "Hapo ndipo wanawake wanapokwenda kuacha mibili yao". Neno Muhimbili likazaliwa hivyo, nalo ladumu hadi leo.
Kwa leo hii Muhimbili ina shule ya madaktari, wauguzi, mafamasia, waganga wa meno, maafisa afya mazingira, maafisa mazingira na elimu ya juu ya afya.
Chuo kikuu cha Muhimbili kilianzishwa mwaka 1963, kilifunguliwa kama chuo cha afya Dar es Salaam ndani ya hospitali iliyoitwa Princess Margaret Hospital na wanafunzi 10 waliofuata kozi za uganga au upasuaji.
Mwaka 1968 kikafanywa ni kitengo cha tiba katika Chuo kikuu cha Dar es salaam.
Tangu 2007 imeandikishwa kama Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili.
Ndani ya chuo kuna idara nne na taasisi tano.
Idara nne ni kama zifuatazo:
Kati ya taasisi kuna taasisi za afya ya umma na uganga wa kimila.
Mpaka mwaka 2018, chuo kina matawi mawili:
{{cite web}}
: Unknown parameter |=
ignored (help)
{{cite web}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help); Unknown parameter |=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Kigezo:Vyuo vikuu vya Tanzania
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Muhimbili kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |