DJ Pooh | |
---|---|
Jina la kuzaliwa | Mark Jordan |
Amezaliwa | 29 Juni 1969 Los Angeles, California, United States |
Kazi yake | Mtayarishaji rekodi, rapper, mwigizaji wa sauti |
Miaka ya kazi | 1984 - hadi sasa |
Ameshirikiana na | King Tee, Chilly Chill, Kam, Ice Cube, Dr. Dre, Snoop Dogg |
Mark Jordan (amezaliwa 29 Juni, 1969 mjini Los Angeles, California), anajulikana zaidi kwa jina lake la kisanii kama DJ Pooh ni mtayarishaji wa rekodi za muziki wa hip hop kutoka nchini Marekani,[1]mwigizaji wa sauti, mghani, mwandishi muswaada andishi,[2] mwigizaji na mwongozaji wa filamu.[3][4] Anafahamika sana kwa uhusika wake kama "Red" katika filamu ya kwanza ya "Friday" ambayo alicheza na Ice Cube. DJ Pooh alishiriki kuandika "Friday" na alisaidia ujenzi wa wahusika katika filamu hiyo. Akiwa kama mkongwe wa kuchanganya madude katika muziki, amewahi kutayarisha albamu wasanii mbalimbali ikiwa ni pamoja na Ice Cube, Del tha Funkee Homosapien, LL Cool J, Yo-Yo, Tha Dogg Pound , King Tee, na wengine kibao. Mwaka wa 1996, DJ Pooh alitoa msaada wa nguvu katika utayarishwaji wa albamu ya pili ya Snoop Dogg, Tha Doggfather. Albmu ilitunukiwa platinamu maradufu.
Taarifa za albamu |
---|
Bad Newz Travels Fast
|
{{cite web}}
: CS1 maint: numeric names: authors list (link)