David Helvorg

David Helvarg (alizaliwa Aprili 10, 1951) ni mwanahabari wa Marekani na mtetezi wa mazingira. Yeye ni mwanzilishi na raisi wa shirika la kupambana na uharibifu wa baharini la Blue Frontier Campaign. Pia ni mshiriki wa Seaweed rebellion harakati isiyo rasmi ya wapinga uharibifu wa mazingira ya baharini. Yeye ni mwandishi; maandiko yake mara nyingi yanahusiana na shughuli za kupambana na uharibifu wa mazingira ya baharini, kama vile kitabu chake cha pili, Blue Frontier. Kitabu chake cha kwanza, The War against the Greens, kinadai kuwa upinzani wa kikatili unaratibiwa dhidi ya harakati za mazingira.

Helvarg alianza kazi yake kama mwanahabari huru, kisha akawa mwandishi wa habari za vita, na hatimaye akarudi katika uandishi wa habari za kawaida. Anaandika kuhusu siasa, UKIMWI, na maisha ya baharini. Ameandika karibu kila bara na ameandika kwa wingi. Uzoefu wake kuhusu migogoro ya kijeshi, migogoro ya kiraia na biolojia ya baharini ndio msingi wa shughuli zake za kupambana na uharibifu wa mazingira.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu David Helvorg kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.