Desmodium intortum | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Majani na maua
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Desmodium intortum, pia inajulikana kama karanga mwitu majani-kijani (kwa Kiing. greenleaf desmodium), ni spishi ya mmea inayotoa maua iliyo kwenye familia (biolojia)familia ya Fabaceae yenye asili ya Mexico, Amerika ya Kati, kaskazini mwa Amerika ya Kusini, visiwa vya Galapagos, Haiti na Jamaika.
Mmea huu umesambazwa maeneo mengi ya kitropiki duniani yakiwemo Afrika, Uhindi, Australia, Nyugini na Taiwan. Ni mmea ambao unaweza kuchakata nitrojeni kutoka kwenye hewa na kuwa kwenye mfumo unaoweza kutumika na mimea kwenye udongo. Pia hutumia kama malisho ya mifugo[1].
Desmodium intortum inatumika kwenye teknolojia ya sukuma-vuta ambapo hupandwa katikati ya muhindi na mtama] ili kufukuza wadudu waharibifu kama vile funza wa mabua (stemborers) na viwavijeshi pamoja na Desmodium uncinatum. Spishi hizi mbili za Desmodium pia zinasaidia kupambana na magugu nyonyaji yaitwayo maguguchawi (Striga) hasa Striga hermonthica na Striga asiatica[2] [3].
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)