Dina Grunitzky alikuwa ni mke wa raisi wa kwanza wa nchi ya Togo Sylvanus Olympio kati ya miaka ya 1961 mpaka 1963 [1]
Alizaliwa mnamo mwaka 1903[2] katika familia ya watoto watatu ambao walikuwa ni Felix na Nicholas Grunitzky.Nicholas Grunitzky yeye alikuwa ni mwanasiasa ambaye alikuja kuwa Raisi wa pili wa nchi ya Togo. Baba yao alikuwa ni Harry Grunitzky ambae alikuwani ni afisa wa kijerumani mwenye asili ya kipolishi na mama yao Hodjinga kutokea kete.
Mnamo mwaka 1930[3] Dina Grunitzky aliolewa na Sylvanus Olympio na wawili hawa walijaliwa kupata watoto watano ambao ni Herbert ambae alifariki mnamo mwaka 1994 wengine ni Ablavi Rosita, Kwami Gilchrist Sylvanus Olympio, Ayaba Sylvana and Kodzo Elpidio Fernando[4][5]
Mnamo mwaka 1963 januari 13 Dina Grunitzky na mumewe Sylvanus Olympio walivamiwa nyumbani kwao na jeshi la watu waliokuwa wakifanya mapinduzi nchi na kuuwawa.
![]() |
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Dina Grunitzky kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |