Eobani na wenzake Adelari, Vintrungi, Valteri, Amundi, Shibaldi, Bosa, Vakari, Gundekari, Eluri na Atevulfi na pengine 41 zaidi (waliuawa Dokkum, katika Uholanzi wa leo, 5 Juni 754) walikuwa askofu, mapadri, mashemasi na wamonaki Wabenedikto waliotumwa kama mmisionari kwa Wafrisia, wakauawa pamoja na Bonifas.
Eobani alikuwa askofu, Adelari, Vintrungi na Valteri mapadri, Amundi, Shibaldi na Bosa mashemasi, Vakari, Gundekari, Eluri na Atevulfi wamonaki tu[1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Kanisa Katoliki na wengineo kama watakatifu.
Sikukuu yao ni tarehe 5 Juni ya kila mwaka[2].
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |