Esuperi wa Toulouse (Arreau, Haute-Pyrénées, Ufaransa, karne ya 4 - Blagnac, Haute Garonne, 411 hivi[1]) alikuwa kwa miaka kadhaa askofu wa mji huo ambao aliupigania usalama wake dhidi ya wavamizi mbalimbali[2].
Alisifiwa na Jeromu, aliyesimulia alivyokuwa anajinyima ili kukarimu wengine, na Gregori wa Tours, aliyesema alikuwa kati ya maaskofu bora wa wakati wake[3].
Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu[4].
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 28 Septemba[5][6].
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |