Forum for the Restauration of Democracy

Forum for the Restauration of Democracy (FORD) ilikuwa kwanza harakati halafu chama cha kisiasa nchini Kenya.

Chanzo 1991

[hariri | hariri chanzo]

Ilianzishwa mwaka 1991 na wanasiasa waliopinga mfumo wa chama kimoja na utawala wa KANU chini ya rais Daniel arap Moi. Shabaha ilikuwa mabadiliko ya kuruhusu vyama vingi na uhuru wa kidemokrasia. Wakati ule chama cha pekee kilichoruhusiwa kilikuwa KANU. Mfumo wa chama kimoja uliporomoka katika nchi nyingi za dunia baada ya mwisho wa ukomunisti na mabadiliko yaliyokwenda sambamba na mwisho wa vita baridi katika Afrika.

Waanzilishi

[hariri | hariri chanzo]

Kati ya waanzilishaji walikuwa Jaramogi Oginga Odinga, Kenneth Matiba, Martin Shikuku, Masinde Muliro na Michael Wamalwa. Mwanzoni FORD ilipigwa marufuku lakini baadaye Moi alilazimishwa na nchi za nje walisaidia sehemu kubwa ya mapato ya serikali kukubali kuwepo kwa FORD.

Mwaka 1992 KANU ilikuwa tayari kubadilisha katiba ya kuruhusu vyama vingi. Walioanzisha vyama mara moja walikuwa Odinga aliyeandikisha FORD kama chama na Mwai Kibai aliyeandikisha Democratic Party (DP). FORD ilikuwa mwanzoni chama cha upinzani wa kitaifa wakati DP ilikuwa na nguvu katika maeneo ya Wakikuyu hasa.

Farakano 1992 juu ya uongozi

[hariri | hariri chanzo]

Swali la nani atakuwa mgombea wa urais likaleta farakano kati ya Matiba na Odinga pamoja na wafuasi wao. Odinga aliondika kabla ya uchaguzi akianzisha chama cha Ford-Kenya na Matiba alibaki na Ford-Asili. Wamalwa pamoja na sehemu kubwa ya viongozi wa Waluhya alishikamana na Odinga. Farakano la Ford-Asili mwaka 1997 likaleta chaama cha tatu cha Ford-People[1].

Farakano hili lilihakikisha kushindwa kwa upinzani katika uchaguzi. Moi hakupata kura nyingi jula la kura 1,927,640 tu. Lakini kura zaidi ya milioni tatu za upinzani ziligawiwa kwa kundi zote tatu yaani Matiba (FORD-Asili) alimaliza na kura 1,354,856 votes, Kibaki (Democratic Party) na kura 1,035,507 na Odinga kwenye nafasi ya nne mwenye kura 903,866.

FORD ilibaki na sifa ya kihistoria ya kufungua milango ya demokrasia nchini kenya lakini haikufaulu mipango mengine.

  1. Will Nyoike sell Nyachae? Nation 13-05-2002