Fátima Djarra Sani | |
---|---|
| |
Alizaliwa | 1968 |
Nchi | Guinea Bisau |
Kazi yake | mwanaharakati wa haki za wanawake |
Fátima Djarra Sani (alizaliwa 1968) ni mwanaharakati wa haki za wanawake nchini Guinea Bissau anayepinga ukeketaji wa wasichana.
Fátima Djarra Sani alizaliwa Bissau, mji mkuu wa nchi, mwaka 1968.[1] Ni mwanaharakati dhidi ya ukeketaji wa wanawake katika nchi ya Guinea Bisau na mwakilishi wa shirika la Médecins du Monde Afrika.[2]
Mwaka 2008, alijiunga na Médecins du Monde, na aliendesha warsha na mafundisho mengine kuhusu hali ya wanawake katika Afrika. Alikazia hasa maswali ya afya ya uzazi na kupinga ukeketaji.[3]
Alishiriki kuandaa itifaki kupinga na hatua dhidi ya ukeketaji wa wanawake ambao ulipata kibali juni 2013 huko Navarra, Hispania.
Mwaka 2015 alichapisha Indomable: de la mutilación a la vida (Indomitable: From Mutilation to Life), na Nyumba ya uchapaji ya Ediciones Península, ambayo alizungumza kuhusu maisha yake.[4]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Fátima Djarra Sani kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |