Gadiel Michael

Gadiel Michael Mbaga ,(amezaliwa Dar es Salaam, 12 Juni 1996) ni mchezaji wa kandanda (mpira wa miguu) ambaye anacheza nafasi ya beki wa kushoto katika timu maarufu katika nchi ya Tanzania ambayo ni Simba S.C.

Gardiel Michael aliwahi kuchezea Yanga msimu wa (2018/2019) akitokea Azam F.C. ambayo yenyewe ilimkuza kupitia akademia yao iliyoibua nyota mbalimbali.

Pia ameichezea klabu ya Singida Fountain Gate (zamani ikijulikana kama Singida United F.C.).

Kwa sasa anaichezea klabu ya Cape Town Spurs inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gadiel Michael kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.