Monoclonal antibody | |
---|---|
Aina | Whole antibody |
Chanzo | Binadamu |
Lengo | IL23 |
Data ya kikliniki | |
Majina ya kibiashara | Tremfya |
AHFS/Drugs.com | Monograph |
MedlinePlus | a617036 |
Taarifa za leseni | US Daily Med:link |
Kategoria ya ujauzito | B1(AU) |
Hali ya kisheria | Prescription Only (S4) (AU) POM (UK) ℞-only (US) |
Njia mbalimbali za matumizi | Chini ya ngozi |
Vitambulisho | |
Nambari ya ATC | ? |
Data ya kikemikali | |
Fomyula | C6402H9864N1676O1994S42 |
Guselkumab, inayouzwa kwa jina la chapa Tremfya, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa ngozi kavu iliyoinuka yenye kuwasha na iliyo na mabaka (plaque psoriasis).[1][2] Dawa hii inatumika kwa ugonjwa wa wastani hadi mkali.[1] Inatolewa kwa sindano chini ya ngozi.[1]
Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maambukizi ya sehemy ya juu ya njia ya upumuaji.[1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha maambukizi, maumivu ya kichwa, maumivu ya viungo, matatizo ya ini na kupungua kwa ufanisi wa chanjo.[3] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[3] Dawa hii ni kingamwili ya monokloni ambayo inashikamana na kuzuia interleukin-23.[1]
Guselkumab iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani na Ulaya mwaka wa 2017.[3][1] Nchini Uingereza, iligharimu Huduma ya Afya ya Kitaifa (NHS) takriban £2,250 kwa miligramu 100 kufikia mwaka wa 2021.[4] Kiasi hiki nchini Marekani ni takriban dola 11,600 za Marekani.[5]
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)