Gwido Maria Conforti (Parma, 3 Machi 1865 – Parma, 5 Novemba 1931) alikuwa askofu mkuu mmojawapo wa Kanisa Katoliki kaskazini mwa Italia.
Kama mchungaji mwema, daima alikesha kulinda Kanisa na imani ya watu wake. Alisifiwa kwa kutembelea mara tano parokia 300 za jimbo lake na kwa kuinua vijana kwa malezi.[1]
Akisukumwa na ari kwa uinjilishaji wa mataifa yote, alianzisha shirika la Wamisionari Wasaveri (tarehe 3 Desemba 1895)[2].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri mwaka 1996 na Papa Benedikto XVI alimtangaza mtakatifu mwaka 2011.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[3].
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |