Isaac L. Auerbach (Oktoba 9, 1921- Disemba 24, 1992)[1] alikuwa miongoni wa waanzilishi na watetezi wa teknolojia za kompyuta anayeshikilia hataza 15. Alikuwa rais mwanzilishi wa Shirikisho la Kimataifa la Uchakataji wa Habari (IFIP) kuanzia mwaka 1960 hadi 1965[2][3], mwanachama wa National Academy of Sciences, mkurugenzi kwenye shirika la Burroughs na mvumbuzi wa kompyuta za awali za Sperry Univac. IFIP lilianzisha tuzo kwa jina lake.