Izates II (Kigiriki: Ἰζάτης, Kiebrania: זוטוס בן מונבז; takriban mwaka 1 – 54) alikuwa mfalme wa Adiabene, ufalme mteja wa Parthia, kutoka takriban mwaka 30 hadi 54.[1]
Anajulikana kwa kugeukia dini ya Uyahudi. Alikuwa mwana wa Malkia Helena wa Adiabene na Monobaz I wa Adiabene. Inasemekana pia kuwa Malkia Helena alikuwa mke wa Mfalme Abgarus wa Edessa na hivyo kuwa malkia wa Edessa pia.[2]
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Izates II kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |