Jimbo Kuu la Tororo (kwa Kilatini Archidioecesis Tororoensis) ni mojawapo kati ya majimbo 20 ya Kanisa Katoliki nchini Uganda na kama hayo yote linafuata mapokeo ya Kiroma.
Kikanisa lina majimbo ya Jinja na Kotido, Moroto na Soroti chini yake.
Askofu mkuu wake ni Emmanuel Obbo, A.J..
Eneo ni la kilometa mraba 8,837, ambapo kati ya wakazi 3.928.600 (2014) Wakatoliki ni 816,200 (20.8%).