Johnny Tri Nguyen | |
---|---|
| |
Jina la kuzaliwa | Johnny Tri Nguyen |
Alizaliwa | 16 Februari 1974 Vietnam |
Mahusiano | Ngo Thanh Van |
Johnny Tri Nguyen (kwa Kivietnam: Nguyễn Chánh Minh Trí, amezaliwa 16 Februari 1974 katika mkoa wa Binh Duong, Vietnam ya Kusini) ni mwigizaji wa filamu, tamthilia, "stunt" na vilevile sanaa ya mapigano wa Kivietnam-Kimarekani.
Johnny aliondoka nchini Vietnam akiwa na umri wa miaka 8 akiwa pamoja na familia yake, mama, baba, kaka, na dada: wote wakaelekea zao jijini Los Angeles. Johnny ni nusu Mchina kwa kuwa mama yake ni Mchina.
Johnny Nguyen ametoka katika familia yenye asili ya uigizaji. Mjomba wake ni Nguyen Chanh Tin, mwigizaji filamu wa zamani wa Kivietnam, wakati kaka yake ni Charlie Nguyen, ambaye amewahi kuongoza filamu nyingi maarufu za kampuni ya Van Son Entertainment videos.
Filamu alizocheza Johnny ni kama vile Tom-Yum-Goong (ya Tony Jaa) na Cradle 2 the Grave. Kazi za ustant[1] kacheza katika filamu ya Spider-Man sehemu ya pili na alicheza kama Green Goblin katika sehemu za mwanzomwanzo. Johnny ni mtaalamu wa kupambana kwa Kung fu, Wushu , Tai chi, Aikido, na vovinam.