José Trinidad Sepúlveda Ruiz-Velasco (30 Machi 1921 – 4 Septemba 2017) alikuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini Meksiko.
Alizaliwa huko Atotonilco El Alto, Meksiko, akapadrishwa tarehe 27 Machi 1948. Sepúlveda Ruiz-Velasco aliteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la [[Tuxtla Gutiérrez\\ mnamo Mei 20, 1965, na akapewa daraja la uaskofu tarehe 25 Julai 1965. Mnamo Februari 12, 1988, alihamishiwa kuwa Askofu wa Jimbo la San Juan de los Lagos, ambapo alihudumu hadi alipostaafu tarehe 20 Januari 1999.
Alifariki dunia tarehe 4 Septemba 2017 kutokana na matatizo ya kupumua akiwa na umri wa miaka 96.[1]
![]() |
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |