Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)

"Deutsches Kolonial-Lexikon" ni jina la Kijerumani la "Kamusi ya Kikoloni ya Kijerumani" iliyotolewa mwaka 1920. Kamusi hiyo ilikusanya habari juu ya koloni zote za Ujerumani kabla ya 1914.

Kamusi imepita kipindi cha hakimiliki ikawekwa mtandaoni kama programu huria. Ni rejeo muhimu la habari za kihistoria kuhusu nchi zilizokuwa chini ya Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia kama vile Tanzania, Rwanda, Burundi, Kenya (Witu), Namibia, Togo na Kamerun barani Afrika na maeneo ya Pasifiki kama Samoa, Guinea Mpya na visiwa vya Mariani halafu Tsingtao (Uchina).

Kamusi iliandikwa kwa lugha ya Kijerumani na wataalamu wa jiografia, biolojia, uchumi, lugha na masomo mengine mengi wenye ujuzi kuhusu nchi waliozieleza katika kamusi. Kuna takwimu nyingi katika makala za kamusi hii.

Katika mambo ya utamaduni na historia inapaswa kusoma makala yake kwa uangilifu. Mara nyingi itikadi ya ubaguzi wa rangi iko wazi kabisa pamoja na dharau kwa wenyeji wa koloni hizi. Hata hivyo mwanahistoria ataitumia kama kumbukumbu muhimu.

Kamusi ilikuwa tayari MWAKA 1914 lakini haikuchapishwa kwa sababu ya Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Kuchapishwa kulitokea baada ya vita kwisha tu. Mhariri alikuwa Heinrich Schnee aliyewahi kuwa gavana wa mwisho wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

Kamusi inapatikana mtandaoni kwenye anwani: Deutsches Koloniallexikon Ilihifadhiwa 9 Desemba 2008 kwenye Wayback Machine.