Kianuak ni lugha ya Kinilo-Sahara nchini Ethiopia na Sudan Kusini inayozungumzwa na Waanuak. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kianuak nchini Ethiopia imehesabiwa kuwa watu 88,000. Nchini Sudan Kusini kuna wasemaji 52,000 (1991). Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kianuak iko katika kundi la Kinilotiki.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kianuak kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |