Kibentong (pia Kidentong) ni lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia inayozungumzwa na Wabentong kwenye kisiwa cha Sulawesi. Mwaka wa 1987 idadi ya wasemaji wa Kibentong imehesabiwa kuwa watu 25,000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kibentong iko katika kundi la Kisulawesi-Kusini.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kibentong kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |