Kiolrat ni lugha ya Kiaustronesia nchini Vanuatu inayozungumzwa na Waolrat kwenye kisiwa cha Gaua. Mwaka wa 2008 idadi ya wasemaji wa Kiolrat imehesabiwa kuwa watu watanu tu, yaani lugha imekaribia kutoweka kabisa hivi karibuni, sababu yake kuwa Waolrat wengi wamebadilisha lugha na kutumia Kilakon badala ya lugha yao ya Kiolrat. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiolrat iko katika kundi la Kioseaniki.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiolrat kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |