Kiserua ilikuwa lugha ya Kiaustronesia nchini Indonesia iliyozungumzwa na Waserua kwenye kisiwa cha Serua. Hakuna wasemaji wa Kiserua siku hizi. Waserua wote walihamishwa na serikali kutoka kisiwa chao cha Serua kwa sababu ya madhara ya kivolkeno, wakapoteza lugha yao na kutumia lugha nyingine wakiishi kisiwani kwa Seram sasa. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kiserua iko katika kundi la Kitimor-Babar.
Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Kiserua kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |