Kyaka

Kyaka ni kata ya Wilaya ya Missenyi katika Mkoa wa Kagera, Tanzania, yenye postikodi namba 35312 [1].

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 16,882 [2]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 13,190 waishio humo.[3]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kyaka iko upande wa kusini wa mto Kagera. Kutoka huko kuna daraja linalounganisha sehemu ya mkoa upande wa kaskazini wa mto Kagera. Wakati wa vita vya Kagera jeshi la Uganda lilivamia maeneo upande wa kaskazini wa mto wakajaribu kuvunja daraja la Kyaka kwa mabomu ya ndege za vita. Hiyo ilishindikana kwa hiyo wataalamu kutoka migodi ya Kilembe walifaulu kubomoa daraja kwa kutumia baruti kali mwanzo wa Novemba 1978[4]. Daraja likajengwa upya baada ya vita.

  1. "Nakala iliyohifadhiwa" (PDF). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
  2. https://www.nbs.go.tz, uk 177
  3. Sensa ya 2012, Kagera - Missenyi District Council
  4. Mwakikagile, Godfrey (2010). "Nyerere and Africa: End of an Era". New Africa Press. Iliwekwa mnamo 16 Machi 2013. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |1= (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Kata za Wilaya ya Missenyi - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Bugandika | Bugorora | Buyango | Bwanjai | Gera | Ishozi | Ishunju | Kakunyu | Kanyigo | Kashenye | Kassambya | Kilimilile | Kitobo | Kyaka | Mabale | Minziro | Mushasha | Mutukula | Nsunga | Ruzinga

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kyaka kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.