Lehlogonolo "Hlogi" Sechaba Tholo (alizaliwa tarehe 12 Desemba 1992) ni mchezaji wa mpira wa kikapu nchini Afrika kusini kwenye klabu Cape Town Tigers pia na timu ya taifa nchini humo.
Msimu wa 2021, Tholo allicheza timu ya Soweto Panthers. Akiwa na timu iyo, alifika fainali ya BNL na rekodi yake ya pointi 25, rebaundi 5 katika pasi 7.[1] Nakutangazwa kuwa MVP wa mchezo.[2]
Tangu 2021, Tholo yuko kwenye orodha ya wachezaji wa Cape Town Tigers.[3]
Tholo alichezea timu ya taifa, Afrika kusini katika mashindano ya AfroBasket mwaka 2017. Mchezo wa pili dhidi ya Msumbiji alifunga pionti 12.[4]