Lumateperoni

 

Lumateperoni, yaani, Lumateperone, inayouzwa chini ya jina la chapa Caplyta, ni dawa inayotumika kutibu skizofrenia (ugonjwa unaoathiri uwezo wa kufikiri, kuhisi na kutenda kwa uwazi).[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[2]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na usingizi na kinywa kavu. [1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha ugonjwa mbaya wa neuroleptic, dyskinesia ya kuchelewa, kisukari, kuongezeka kwa uzito, chembechembe nyeupe za damu, kifafa, na uratibu duni.[2] Huongeza hatari ya kifo kwa wazee wenye shida ya akili.[2] Ni dawa ya kutibu akili isiyo ya kawaida.[2]

Iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2019.[1] Nchini Marekani, inagharimu takriban USD 1,400 kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[3]

Marejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. 1.0 1.1 1.2 "Lumateperone Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 19 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Caplyta- lumateperone capsule". DailyMed. Intra-Cellular Therapies, Inc. 27 Desemba 2019. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Julai 2020. Iliwekwa mnamo 3 Julai 2020.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Lumateperone Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Januari 2024. Iliwekwa mnamo 24 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)