Madina Nalwanga (alizaliwa Februari 2, 2002)[1] ni mwigizaji wa kutoka Uganda ambaye anajulikana sana kwa kucheza uhusika wa Phiona kwenye filamu ya Disney's iitwayo Queen of Katwe.[2] Filamu inaelezea maisha ya Phiona Mutesi, mdada waUganda anayeishi kwenye kitongoji duni cha Katwe alijifunza kucheza sataranji mpaka kufikia kuwa Woman Candidate Master.[3] uhusika huu kwenye hii filamu ulimfanya ashinde Most Promising Actor ya mwaka 2017 Africa Movie Academy Awards kule Lagos, Nigeria.[4] alishinda pia NAACP Image Award, ya Women Film Critics Circle Award, na aliteuliwa kwenye Critic's Choice Award.[5]
Madina alizaliwa kwenye Kijiji duni cha Katwe kilichopo Kampala, Uganda, alitumia utoto wake kuuza mahindi mtaani.[6] Nalwanga aligundulika na muongozaji filamu kwenye ngoma ya jamii Kabalagala neighborhood ya Kampala, Uganda, Kijiji kinachojulikana kwa umalaya.[7][8]
Wakati wa kutengeneza filamu ya Queen of Katwe, David Oyelowo aliwapeleka Nalwanga kuona Jurassic World Pamoja na watoto wengine, na aligundua hajawahi kuona filamu pale alipouliza, "ndo hicho tunachokifanya?"[9] Alipoangalia Queen of Katwe, ndo ilikua mara yake ya pili kuwepo ndani ya ukumbi wa sinema.[10]Alisema Maisha yake ya utoto yanaelezewa kwa karibu na uigizaji wake kama Phiona kwenye Queen of Katwe.[6] Akiwa na miaka 17 jarida la Forbes lilimtaja kama mtu mwenye umri mdogo kwenye orodha yao ya 2018 ya “30 under 30” [11] kutokana na kisomo cha University of Oxford kupitia idara ya uchumi, wanafunzi wa Uganda walioangalia Queen of Katwe kabla ya kwenda kufanya mitihani yao ya taifa walipata madaraja mazuri Zaidi kuliko ambao hawakuangalia. [12][13]
{{cite web}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)
{{cite web}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)
{{cite news}}
: More than one of |accessdate=
na |access-date=
specified (help)