Magadi ni mji uliopo kando ya Ziwa Magadi upande wa mashariki, katika Bonde la Ufa la Afrika Mashariki. Pia mji wa Magadi upo kaskazini mashariki mwa Ziwa Natron in Tanzania.[1]
Magadi ni kata ya Eneo bunge la Kajiado Magharibi, nchini Kenya[2].
Magadi ni makao makuu ya kaunti ndogo ya Magadi katika kaunti ya Kajiado. Kampuni ya Magadi Soda Company ipo katika mji huu.
Idadi ya watu wanaoishi Magadi ni 980 (sensa ya 1999) na kimo juu ya usawa wa bahari ni mita 595 [3]
Magadi imepata huduma za mtandao, na matumizi ya kompyuta, kwa njia ya Unite Nations Development Program-Kenya kwa ajili ya kompyuta zinazotumia nguvu ya jua. Mpango huu ulianza Julai 2002: na mwisho wa 2003, zaidi ya wakazi 10,000 (48%) walikuwa wametembelea vituo tano vya huduma za mtandao.[4]
Mji wa Magadi ulitumiwa katika filamu ya Fernando Meirelles ya The Constant Gardener.
1°53′S 36°16′E / 1.883°S 36.267°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Magadi, Kenya kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |