Makunduchi ni mji wa Tanzania, ulioko kwenye sehemu ya kusini mashariki ya Unguja, kusini mwa Jambiani, katika Wilaya ya Kusini ya Mkoa wa Unguja Kusini. Maeneo yake yamegawiwa kwa shehia za Kijini, Kiongoni, Mzuri, Nganani na Tasani.
Mji una makazi mawili tofauti, takriban kilomita 2 kutoka kwa kila mmoja, "Makunduchi ya Kale" na "Makunduchi Mpya". Old Makunduchi ni kijiji cha wavuvi wadogo, wakati New Makunduchi ina majengo ya kisasa, maduka, pamoja na baadhi ya vitalu vya gorofa vilivyojengwa miaka ya 1970 kwa msaada wa fedha na wahandisi wa Ujerumani Mashariki.[1]
Kulikuwa mahali pa makazi ya Waswahili wa kale katika pwani ya Bahari ya Hindi.
Makunduchi ni maarufu kwa sikukuu ya Mwaka Kogwa[2] (pia Mwaka Koga[3] na Siku ya Mwaka). Ndipo kati ya mahali pachache ambako sikukuu hiyo imehifadhiwa ambayo inahesabiwa katika ya urithi wa Washirazi. Zamani wakazi wa pwani yote ya Afrika ya Mashariki walitumia Kalenda ya Kiswahili ambayo ni kalenda ya Jua pamoja na Kalenda ya Kiislamu[4] lakini tangu siku za ukoloni Kalenda ya Gregori imeenea na kuchukua mahali pake. Hivyo Makunduchi inatunza Siku ya Mwaka kama siku ya kwanza ya mwaka wa Kiswahili. Katika desturi za Makunduchi kuna mapigano ambako mwishoni kibanda kinachomwa. Mwelekeo wa moshi wa moto huchukuliwa kama ishara za matukio ya mwaka unaofuata.[5]
Makunduchi ni eneo lindwa Zanzibar. Hoteli ya kwanza ilijengwa katika ufukwe wa Makunduchi mwaka 2006. [6]
{{cite book}}
: |edition=
has extra text (help)
{{cite web}}
: More than one of |archivedate=
na |archive-date=
specified (help); More than one of |archiveurl=
na |archive-url=
specified (help)