Mary Wambui

Mary Wambui

Mary Wambui ni mfanyibiashara mwanamke wa Kenya na kuna madai kuwa yeye ni mke wa pili wa Rais wa Kenya Mwai Kibaki. Familia ya Wambui inadai kuwa Mwai alimwoa Maria mwaka 1972 chini ya sheria za kimila za Kikuyu na kuwa wana binti, Wangui Mwai.

Kibaki, alitoa taarifa rasmi akisema kuwa mke wake, Lucy Kibaki na watoto wao ndio walikuwa familia yake pekee ya karibu. Ingawa amekanwa kama mke, Wambui hupewa huduma zote za mkewe rais zikiwemo walinzi na magari ya kifahari. [1] Ilihifadhiwa 13 Machi 2007 kwenye Wayback Machine.

Winnie Wangui alihusishwa na sifa mbaya za 'Mandugu wa Artur' kwa njia za kibiashara na kibinafsi. Katika tukio lililopewa jina 'Armenian Saga', 'ndugu hao' (Artur Margaryan na Artur Sargasyan), ambao walikuwa pia wamesemekana kuwa majeshi wa kulipwa, walionyeshana mabunduki katika uwanja wa ndege wa JKIA ndani ya eneo la "usalama" na kutishia kumpiga risasi afisa wa Forodha ambao walitaka kuchunguza mizigo yao. Tukio hili la uvunjaji sheria lilifanya wakamatwe na hatimaye kufukuzwa nchini tarehe 9 Juni 2006. Winnie alifutwa kazi baada ya tukio hili. [2] Ilihifadhiwa 6 Januari 2008 kwenye Wayback Machine.

Katika mahojiano na The Standard yaliyoandikwa tarehe 5 Aprili 2007, Winnie alisema kuwa yeye na Margaryan walikuwa na lengo la kuoana katika siku zijazo. [3] Ilihifadhiwa 23 Januari 2008 kwenye Wayback Machine.

Katika vyombo vya habari vya Kenya, Mary Wambui huitwa "Mwanaharakati wa NARC". Chama cha kisiasa nchini Kenya.

Katika mahojiano ya juzi juzi na vyombo vya habari nchini Kenya, Wambui alisema kwamba yeye alikuwa na watoto watano lakini alisita kuyataja majina yao.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mary Wambui kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.