Micere Githae Mugo (alizaliwa Madeleine Micere Githae; 1942 - 2023) alikuwa mwandishi wa filamu na vitabu na mwanaharakati, muongozaji na mtunzi wa mashairi kutoka Kenya[1]. Alikuwa mhakiki wa kusoma na kuandika na Profesa wa kazi za Fasihi katika Kitengo cha mafunzo ya watu wenye asili ya Afrika katika chuo kikuu cha Syracuse, New York huko Marekani.
Mugo alizaliwa Baricho, wilaya ya Kirinyaga, mwaka 1942, akiwa mtoto wa walimu wawili waliokuwa wakishiriki siasa na kuhusika katika kupigania uhuru wa Kenya. Alisoma katika shule ya msingi na ya sekondari akiwa huko kenya na kusoma katika shule ya Alliance Girls kwenye ngazi ya kidato cha tano na sita[2]. Ndiye mwanafunzi wa kwanza Mweusi kusoma kwenye shule ambayo ilikuwa ikibagua mwanafunzi kwa rangi ya ngozi zao.[3]