Mlima Ayalu (ambao pia unaandikwa Ayelu) ni mlima uliopo mashariki mwa nchi ya Ethiopia, upande wa mashariki wa mto Awash. Mlima huo una latitudo na longitudo za vipimo 10°5′N 40°42′E / 10.083°N 40.700°Ena mwinuko wa mita 2145.
Watu wa Argobba wana utamaduni kila baada ya kufika Afrika katika eneo la Zeila, hutembelea mlima huo kwa miaka mingi na hutazamia mafanikio katika utajiri, ndoa, harusi hata sherehe za ibada mbalimbali wakati wa mwezi wa Ramadhan; na bila kufanya hizo ibada inasemekana Allah huleta mapigo na njaa.[1]
Wilfred Thesiger anauelezea mlima huu wa kale wa Ayalu mwaka 1933. Anaeleza kuwa mlima huu ulikuwa na hija kila mwaka na kila mwanajumuia wa Waafar kutoka mbali Daoe na Aussa ili kupanda kileleni unatakiwa kufanya ibada na kuwa na afya njema kuhimili vita. Pia waliweza kufanya hija mlimani hapo na pia kuombea unafuu, ahueni katika balaa ya njaa na pigo pia baada ya ushindi katika vita.
Makala hii kuhusu maeneo ya Ethiopia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Mlima Ayalu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |