Monica Dawson | |
---|---|
muhusika wa Heroes | |
Dana Davis kama Monica Dawson | |
Mwonekano wa kwanza | "The Kindness of Strangers" |
Mwonekano wa mwisho | "Powerless" |
Imechezwa na | Dana Davis |
Maelezo | |
Majina mengine | Saint Joan |
Kazi yake | Mhudumu Memba wa kamati ya wazalendo |
Uwezo | Kuiga kile anachokiona |
Monica Dawson, imechezwa na Dana Davis, ni jina la uhusika wa tamthilia ya ubunifu wa kisayansi kwenye TV ya NBC , Heroes. Akiwa katika miaka yake ya 20 ya mwanzoni kabisa kutoka mjini New Orleans - anajikuta kuwa na nguvu ya kugezea kitu chochote kinachotembea ilimradi tu akione.
Monica Dawson alikuwa mmoja kati ya wahusika wachache waliojiunga katika msimu wa pili wa mfululizo. Yeye ni wa kwanza katika mabinamu wa Micah Sanders, na ni mpwa wa D. L. Hawkins. Pia ana mdogo wake aitwaye Damon. Anaishi na bibi yake, Nana Dawson, ambaye ndiye anayebeba jukumu zima kumlea Monica na ndugu yake. Monica na familia ya kina Dawason inaishi mjini New Orleans ambayo ilipatwa na mafuriko ya nguvu yaliyotokana na Kimbunga cha Katrina. Inatambulika kwamba mama yake alikufa wakati wa maangamizi yaliyotokana na Kimbunga cha Katrina.[1]
TV Guide wanamweleza Monica kama "malaika wa jioni ambaye amenuia kuleta haki kwa rushwa iliyoenea," huenda ikawa amevutiwa kufanya hivyo kwa kufuatia kifo cha mama yake. Nyumba ya familia yake ilikumbwa na mafuriko, na kuiacha familia yake ikiwa na hali ngumu ya kifedha, bilashaka kumpoteza mama yake kwa ghafula. Anafanyakazi kwa juhudi ili kukimu kimaisha mdogo wake na bibi yake (imechezwa na Nichelle Nichols).
Isitoshe inabidi adili na madhila ya kugundua kama ana nguvu za kipekee. Ni msichana mzuri mwenye moyo mzuri ambaye maisha yake yamechukuliwa kutoka kwake, na anatafuta pa kutokea.[2] Amechukua uhusika wa uangalizi wa mtoto wa Niki na D.L., Micah, ambaye anaishi na familia ya Dawson wakati wa msimu wa pili.