Shirikisho la mpira wa Kikapu nchini Misri Ni Shirikisho la Mpira wa Kikapu Nchi Misri linaloongozwa na baraza la mchezo wa mpira wa vikapu. Ilijiunga na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Kikapu FIBA mnamo mwaka 1934.
Iilianzishwa mnamo mwaka 1934, na walikuwa wanachama wa FIBA Ulaya, kwa vile ukanda wa FIBA Afrika haukuanzishwa hadi 1961.[1]
Ofisi za Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri zinapatikana kairo.
Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri lililenga timu ya taifa ya wanaume ya mpira wa vikapu Nchi Misri, na mafanikio yao yakiwemo nafasi ya 9 katika Olimpiki ya Majira ya mwaka 1952, na nafasi yake ya 5 kwenye Mashindano ya Dunia ya mwaka 1950 FIBA. Katika Mashindano ya FIBA Afrika, Misri inashikilia rekodi ya medali 16. Timu ya wanaume ya Misri ilishiriki Michezo ya Olimpiki ya Majira ya joto mara saba. Katika mwaka 1984 na mwaka 1988, Misri ilikuja katika nafasi ya 12 katika hafla zote mbili.[2]
Timu ya taifa ya mpira wa vikapu ya wanawake ya Misri ilishinda Ubingwa wa FIBA Afrika kwa Wanawake mwaka 1966 na mwaka 1968, na kushika nafasi ya pili mwaka 1970, kama Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu.